copied mwanaspoti
MSHAMBULIAJI Nsa Job Mahenya wa Yanga amesema tatizo la yeye kutokufunga bao hata moja kwenye Ligi Kuu Bara tangu ahamie kikosini humo linamuumiza kichwa. Anasema hana bahati msimu huu, lakini akaongeza kwa kuwatuliza mashabiki wake kuwa hilo lisiwape presha na wanachotakiwa kufanya ni kuangalia uwezo wake anapokuwa uwanjani.
Nsa, mchezaji wa zamani wa Simba, tangu kujiunga kwenye kikosi cha wana- Jangwani mwanzoni mwa Ligi amekuwa akicheza mechi karibu zote za Ligi Kuu, lakini hakuna hata moja aliyowahi kufunga, ukiachilia mbali bao moja la michuano ya Mapinduzi Zanzibar na mechi nyingine za kirafiki.
Mwanaspoti ilimtafuta na kuzungumza naye ili kujua tatizo linalomsumbua na kusema: "Suala la kufunga mimi nashindwa hata kulizungumzia kwa sababu linaniumiza kichwa sana na najiona sina bahati msimu huu Na kama wao (mashabiki) linawauma, mimi ni zaidi kwani napenda mafanikio yangu na klabu kwa ujumla, maana ninapofunga mambo mengine hutokea, lakini ndiyo hivyo linashindikana, anasema Nsa ambaye ni shabiki wa Liverpool ya England. Nimekuwa nikilifikiria sana kwa nini sifungi, lakini nakosa majibu kiasi ambacho sasa sitaki kabisa kuliweka kichwani kwa sababu linaniumiza, anasema Nsa anayezimikia soka la Mreno Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Nikifikiria sana nabaki naumia tu bila mafanikio yoyote, kilichopo sasa na ninachokiangalia ni uwezo wangu, namna gani nitaboresha na kujibiidisha kiwango changu ili kutoa mchango kwa timu yangu. Na ndivyo ninavyowaambia mashabiki wasiwe na hofu kwa kujiuliza maswali mengi, kubwa na la muhimu ni uwezo, waangalie kiwango changu kikosini kwa sababu mchango kwenye timu si kufunga peke yake, yapo mambo mengi,a nasema Nsa anayemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja mwishoni mwa msimu huu Suala la kubadilishwa namba au mambo mengine hilo halipo na jibu ni hilo hilo, msimu huu mimi sina bahati, anaeleza Nsa.
SIMBA, YANGA NA KLABU NYINGINE ALIZOPITA.
Nsa ni mchezaji aliyezichezea klabu mbalimbali za Ligi Kuu zikiwemo kubwa za Simba, Yanga na Azam FC kwa misimu tofauti na amezizungumzia kwa kusema Nimecheza klabu hizo kwa sababu ya maslahi, pamoja na mambo mengine yote, mpira ndio unaoendesha maisha yangu, anasema Nsa aliyezichezea pia Moro United na Twiga. "Namshukuru Mungu huko kote nilikopita nilicheza kwa mafanikio, sikuwa msindikizaji kwa sababu namba ya kucheza nilikuwa napata Changamoto zipo, kama unavyojua, mahali popote penye riziki kuna mambo yake, nimechezea timu hizo nimekutana na mambo mbalimbali na hata hapa nilipo sasa ninayokutana nayo ni makubwa, binafsi siwezi hata kuyazungumza hadharani, lakini kwa sababu nafanya kazi kwa malengo inabidi kuyavumilia, anaeleza Nsa.
MALENGO YAKE
Kubwa la kwanza ninalolifikiria sasa ni kuona natoa mchango wangu wa hali na mali kuhakikisha naisaidia Yanga kutwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, baada ya kukosa kwenye michuano ya Kimataifa, anasema Nsa mzaliwa wa Morogoro mtaa wa Misufini na baba yake ndiye Diwani wa kata hiyo.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Misufini na baadaye akaenda Sekondari ya Forest kidato cha kwanza na cha pili na kumalizia Makongo mwaka 2004. Naamini Yanga bado wana nafasi ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kama mipango yetu itakwenda sawa kama hatutapoteza mchezo hata mmoja wa Ligi kwa sababu mwalimu tuliyenaye, Sam Timbe, ni mzuri japo siwezi kumzungumzia sana wasifu wake kwa sababu ni mapema mno. Kingine, kama unavyojua, kila mchezaji anatamani siku moja na yeye awe wa kimataifa, hilo lipo kwa hiyo kama ndoto yangu itakuwa sawa na mimi nipate timu kubwa na nzuri ya kuichezea nje ya nchi," anaeleza Nsa.
HAPENDI KUONA
Nsa anasema hapendi kusikia wala kuona dharau. Sipendi na sitaki kusikia wala kuona kabisa kitu dharau, hata kama ni kiongozi wangu. Napenda heshima, tuheshimiane, kwa kiongozi au mtu yeyote. Ninapokuheshimu na wewe uniheshimu, lakini kuna wengine hutumia vyeo vyao kuwadharau wengine kutokana na uwezo walionao, anaeleza Nsa aliyeweka wazi kuwa alisajiliwa na Yanga baada ya kocha wa zamani Kostadin Papic kuizimikia soka yake. Watu wote ni sawa, kubwa ni kupendana, kama ni mahali pa kazi kufanya kazi kwa umoja wenye mafanikio.
Amezaliwa Misufini, Morogoro Februari 25 , 1987
Alizichezea Twiga 2004 akiwa Makongo
2005-2007 Moro United
2007-2008 Simba
2008-2009 Moro United
2009-2010 Azam FC
2010-2011 Yanga
0 comments:
Post a Comment