aamsuni
Michuano ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), inataraji kuanza tarehe 19 machi mwaka huu kwa kuwa kutanisha bingwa Business Times na wandaaji NSSF.
Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza zawadi za washindi na kukabidhi vifaa kwa timu shiriki, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha vyombo vya habari, yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya TCC Chang'ombe na Uwanja wa Chuo cha Uwalimu Dar es Salaam (DUCE). Alisema kwa mwaka huu mshindi wa kwanza kwa upande wa soka atapata kombe na sh. milioni 3.5 , wa pili kombe na sh. milioni 2.5 na wa tatu atapata kombe na sh. milioni 1.5 , mfungaji bora kwa upande wa wanawake na wanaume atapata sh. 200 ,000 kila mmoja.
Timu shiriki zimegawanywa katika makundi manne nayo ni:
Kundi A: NSSF, Business Time, mlimani na changamoto.
Kundi B: Radio Heri, Habari zanzibar, new habari na Global.
Kundi C: Mwananchi, Uhuru, Mwanahalisi, Sahara na Tumaini.
Kundi D: Tbc, Jambo leo, IPP, Free media
0 comments:
Post a Comment