aamsuni
Simba sc ya Dar es salaam leo anateremka kiwanjani mjini Lubumbashi kumkabili bingwa mtetezi wa klabu bingwa Africa, TP Mazembe katika mchezo wa klabu bingwa Africa.
Simba wanatarajia kucheza mchezo wa kulinda huku wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Mazembe. Simba wanatarajia kutumia mfumo 4-5-1 huku wakitegemea kasi ya Emanuel Okwi pamoja na Samatta.
Kikosi cha simba kinacho tarajiwa kuanza, kwa mujibu wa mazoezi ya mwisho ni, Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah, Kelvin Yondani, Juma Nyosso, Jerry Santo, Rashid Gumbo/Nico Nyagawa, Patrick Ochan, Emanuel Okwi, Mbwana Samata, Amri Kiemba.
TP Mazembe ambayo inasaka ubingwa wake watatu mfululizo haija poteza mchezo wowote wa michuano klabu bingwa Africa mjini Lubumbashi katika miezi ya hivi karibuni.
Wanafainali hao wa klabu bingwa dunia inataraji kutumia mfumo wa 4-4-2 ambao wamekuwa wakiutumia mara kwa mara. TP Mazembe itakosa huduma za Tresor Mputu aliyefungiwa pamoja na majeruhi Erick Nkulukuta na Stopila Sunzu.
TP Mazembe ita wategemea Mbeza Bedi, Dioko Kaluyituka, Ngandu Kasongo na Given Singuluma, katika mchezo wa leo.
Waamuzi wa pambano hili la leo wote wanatokea nchini Misri. Kunauwezekano wa TBC1 kuoonyesha mpambano huo moja kwa moja (laivu).
0 comments:
Post a Comment