aamsuni
Timu ya simba sc imezidi kujikita kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara, baada ya kuifunga AFC ya mkoani Arusha magoli mawili kwa bila.
Simba ambayo iliwasili Arusha siku ya alhamisi na msisimko wa pambano hilo kuamka na huku kukiibuka uvumi wa simba kurubuni baadhi ya wachezaji wa AFC. Mtafaruku ulitokea baada ya kiingilio kutangazwa ni Tsh 5000, na Tsh 10,000 hali hiyo iliwafanya mashabiki kulalamika, huku wengine waki nunua tiketi.
Hali ya bei ya tiketi ilipelekea mashabiki wengi ambao walikuwa hawaja kata tiketi, watake kuingia bure uwanjani, baada ya tiketi kushushwa bei kuwa Tsh3000 na Tsh5000.
Mpambano ulianza kwa kasi huku simba ikitafuta goli la mapema, ambalo walilipata dakika ya tano baada ya Emanuel Okwi kuachia shuti ambalo kipa alilipangua na kumfanya Ochan afunge kirahisi. Goli la pili lilifungwa na Rashid Gumbo kwa shuti kali lililo mshinda mlinda mlango wa AFC Arusha.
YANGA WAPELEKWA NA GWARIDE
Timu ya jeshi la kunyenga Taifa, Jkt ruvu imeipeleka puta yanga katika mchezo uliochezwa kwenye nyasi bandia za Uhuru. Jkt ruvu inayosifika kwa kumiliki mpira ilipoteza nafasi nyingi ambazo zingeweza kumuumiza yanga sc.
Yanga nao walipoteza nafasi kadhaa, katika mchezo huo wa ligi kuu, ambao ulikwisha kwa sare ya bila kufungana.
Kutokana na sare hiyo yanga inafikisha point 40 wakati Simba sc ikiwa imefikisha point 44 baada ya mchezo wa jana.
0 comments:
Post a Comment