aamsuni
Taifa stars na Harambe stars wamefanikiwa kutoka na ushindi wa magoli mawili kwa moja na hivyo kufufua matumaini ya kufuzu kwend Gabon na Equiteral Guine.
Taifa stars wakiwa mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Taifa, walikipiga na Jamhuru ya Africa ya kati. Jamhuri ya africa wa kati walikuwa wa mwanzo kupata goli katika kipindi cha kwanza. Goli hilo lilimchanganya Shaban Kado ambaye alipelekwa kwenye post. Goli hilo lilidumu kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kuliandamat goli la jamhuri ya afrika ya kati na kufanikiwa kupata goli dakika ya 49 kupitia kwa kiungo wa mtibwa sugar Shaban Nditi.
Wakati mashabiki wananyanyuka kwenye viti huku wakiamini stars wamepoteza matumaini, mchezaji anayekuja kasi Mbwana Samata alishinda goli lake la kwanza kwa timu ya taifa likiwa la ushindi dakika ya 89. Hadi mwisho wa mchezo stars mbili, afrika ya kati moja.
Kutokana na ushindi huo stars wamefikisha point 4 huku akifufua matumaini ya kufuzu kushiriki kombe la mataifa afrika.
Nchini kenya kulikuwa na mpambano mwingine wa kufuzu kwenda Gabon ambapo Kenya waliwakaribisha Angola.
Katika mchezo huo kenya wameibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja magoli ya kenya yakifungwa na Jamal Mohamed pamoja na Mariga.
0 comments:
Post a Comment