zanzibar

Tuchangie soka la Zanzibar kwa maeendeleo ya Taifa stars.

aamsuni
Kwa muda sasa soka la zanzibar linazidi kuzorota, hali hii imepelekea kukosekana mchezaji kutoka ligi ya Zanzibar katika timu ya Taifa stars.
Ligi kuu ya Zanzibar kila msimu upigwa kalenda ya kuanza kutokana na kukosekana wadhamini na hivyo kupelekea vilabu kutoka Zanzibar kubolonga katika mashindano ya kimataifa.
Ukizungumzia kuporomoka au kupanda kwa soka Tanzania lazima Zanzibar uiguse kwani Fifa awajaipa uwanachama Zanzibar na kupelekea kutambulika kama Tanzania.
Tukirudi kwenye miaka ya nyuma ambako Zanzibar walikuwa vizuri kisoka hata upande wa timu ya Taifa stars ambayo ilikuwa na sura ya muungano ulikuwa vizuri. Kuzorota kwa ligi ya Zanzibar na soka lake kwa ujumla kunaiadhiri timu ya Taifa.
Tuungane na Masanja kuichangia soka la Zanzibar kwa mustakabali wa timu ya Taifa stars. Taifa stars ya sasa inakosa sura ya muungano kwa kukosekana wachezaji wanaotoka ligi kuu Zanzibar.
Ni wakati wa vilabu vya Zanzibar pamoja ZFA kuamka, kuitangaza ligi yao kwa lengo la kupata wadhamini wa kudumu.
Ligi kuu ya zanzibar imezalisha nyota kibao waliokuja kutamba na timu ya Taifa, simba, yanga, na hata mtibwa wakiwemo kina Abdallah Juma, Abdi Kassim Babi anaekipiga nchini vetnam. Ukianda kwenye kambi ya timu ya taifa u23 utakutana vipaji kutoka timu za Zanzibar ambao hapo baadae itakuja kupeperusha bendera ya Taifa.
Kuchangia soka la zanzibar ndiko kunyanyuwa kiwango cha soka Tanzania.

About kj

2 comments:

Kijiti Stix said...

zanzibar wanajifanya wajuaji. kwa nini wasaidiwe?

si wao walipinga ligi ya muungano? sasa wanalialia nini? walidhani mpira ni sawa na ngoma ya msewe?

kj said...

Ndio kaka, walipikataa ligi ya muungano kwa dhamira ya kutaka watoe muakilishi moja kwa moja kwenye michuano ya CAF.
Hata hivyo wanaanza kuona haja ya ligi ya muungano ndio maana sasa kombe la mapinduzi kila mwaka wanazidi kuliboresha kwa kuzialika timu zilizo fanya vizuri katika ligi kuu bara na hivyo kuwa na sura ya muungano.
kuna haja ya mabosi wa tff na zfa kukaa pamoja na kujadili suala la ligi ya muungano bira shaka ita amsha hamasa ya ligi kuu, kwa kuwa na timu zitakazo kuwa zinagombani kushiriki ligi hiyo baada ya kukosa nafasi CAF

Powered by Blogger.