VPL

Yanga kujiuliza kwa Ruvu.

aamsuni
Katika mikoa mitatu nchini kutakoa na mitanange ya ligi kuu Tanzania bara. Ambapo mikoa miwili itashuhudia mbio za ubingwa na mmoja kujiepusha kushuka daraja.

Dar es salaam, Uhuru
Katika uwanja wa uhuru yanga watateremka kusaka point tatu kutoka kwa Jkt Ruvu. Yanga ambayo imejikuta ikimwachia mpinzani wake kukali uwongozi wa ligi, katika mwa wiki, itataka kuendelea kufukuzana naye mpaka mwisho wa msimu.
Jkt ruvu ni timu nzuri inayocheza mpira mzuri, maneno hayo aliyasema Sterwat kocha wa azam pale aliposhangaa namna timu yake ilivyopelekeshwa japo walitoka na ushindi. Yanga haitatarajia wepesi wowote katika mechi hii ya leo.

Arusha, S.A. Abeid
Mnyama simba atakaribishwa na timu ya AFC ambayo haina matumaini ya kubaki ligi kuu. Simba inaongoza kwa point 41 ikifuatiwa na yanga 39, inataka ushindi mnono, ili kuendelea kukalia kiti cha uongozi.
AFC imekuwa kapu la magoli pale alipokutana na Azam pamoja na yanga, na kwasasa ipo mkiani.

Songea, Majimaji
Katika dimba la majimaji hii leo kutakuwa na mtanange wa kukwepa kushuka daraja pale timu mbili za mkiani zitakapo kuwa zikipepetana. Mwenyeji Majimaji inayoshika nafasi ya 11 itamkaribisha Ruvu shooting ambayo inashika nafasi ya 10.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.