Mchangani

Youth Moro yaibuka kidedea

aamsuni
Timu ya soka ya Moro youth imeibuka bingwa wa wilaya ya Morogoro Mjini baada ya kuifunga shule ya sekondari Mwembesongo magoli matatu kwa moja.
Bingwa wa mashindano hayo wa vijana ambaye ni Moro youth imetwaa kitita cha Tsh 25,000, mshindi pili ambao ni shule ya Mwembesongo wamezoa Tsh 20,000 na watatu Shibobo fc wamepokea Tsh 10,000.
Mashindano haya yaliyofikiwa tamati jumamosi yalikuwa na dhamira ya kusaka timu ya wilaya ya Morogoro Mjini, ambapo vijana 45 na hapo baadae watachujwa kupata timu itakayo wakilisha wilaya katika mashindano ya chini ya miaka 17 ya mkoa wa Morogoro.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.