Mshambuliaji toka Ghana anagombaniwa na klabu ya Simba pamoja na Yanga, Kenneth Asamoah ametua nchini kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya yanga.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage alithibitisha ujio wa mchezaji huyo toka Ghana pale alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hiyo jana.
Rage alisema Asamoah amekuja kwa ajili ya kukutana na uongozi wa klabu ya Yanga. Rage aliwanasi wapinzani wake kufuata taratibu za usajili kama kweli wanataka kumtumia msimu ujao. “Sisi Simba tunazungumza na klabu kama kanuni zinavyoeleza masuala ya kuzungumza na mchezaji moja kwa moja ni makosa kwa mujibu wa kanuni hizo za Fifa hivyo kama kweli wenzetu (Yanga) wanamtaka basi wafanye hivyo,” alisema Rage.
Asamoah alitua nchini kwa mara ya kwanza mwaka jana na kujiunga na klabu ya yanga kwa uwamisho wa dola za marekani 30,000, hata ivyo aliishia kucheza michezo ya kirafiki baada ya usajili wake kuleta utata.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment