vilabu

Birmigham wakubali kutua nchini

Mabingwa wa Carling Cup, Birmingham city wamekubali kuja nchini baada ya kuridhishwa na viwango vya hoteli, hospitali na uwanja wa taifa ambavyo walikuja kuvikagua.
Kocha msaidizi wa Birmingham City Andy Watson na daktari wa timu hiyo, Ian Mc Guiness, wameelezea kuvutiwa na mambo mbalimbali ikiwamo mandhari ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Watson na Guiness juzi walitembelea na kukagua Uwanja wa Taifa, hospitali za Aga Khan, Muhimbili na Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, ikiwa ni maandalizi ya ziara yao ya michezo miwili ya kirafiki hapa nchini dhidi ya Simba na Yanga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Watson alibainisha kuwa wamefanikiwa kuja Tanzania kutokana na matangazo ya utalii yanayo onekana katika uwanja wa Newcastle united, ambapo watatembele vivutio hivyo katika ziara yao hiyo.Aidha, Watson alibainisha sababu za wachezaji wa Tanzania kushindwa kucheza soka barani Ulaya, kuwa ni pamoja na Tanzania kuwa katika nafasi zaidi ya 70 katika viwango vya Shirikisho la Kimataifa (FIFA), ikiwa ni utaratibu wa bara hilo na nchi nyingine zilizoendelea. Alisema ili wachezaji wa nchi kama Tanzania kucheza barani Ulaya, inatakiwa wawe na uzoefu katika timu zao za taifa na vipaji vya hali ya juu, jambo litakalosaidia kushawishi klabu za Ulaya.
Kocha huyo alisema wanatarajia kuwa na msafara wa wachezaji 25 sambamba na watu wengine 1 ,000 ingawa awali waliomba msafara wao uwe na watu 5 ,000.Naye Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema michezo hiyo itatumika kwa ajili ya kuitangaza Tanzania katika masuala ya utalii. Rage alisema katika harakati za kutangaza utalii wa Tanzania, wachezaji wa Birmingham watatembelea Hifadhi ya Serengeti, wakati waliobaki watakwenda mbuga ya Mikumi.
Pia mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba radhi watani wao wa jadi Yanga, kwa kutowapa taarifa kuhusu ujio wa timu hiyo, ambayo itaitangaza Tanzania nje ya mipaka ya nchi sambamba na kufanikisha maendeleo ya soka ya nchi hii.

aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.