Klabu ya soka ya Simba imezidi kunufaika katika mauzo ya wachezaji baada ya Patrick Ochan kusajiliwa na TP Mazembe kwa kitita cha dola 100,000 ( milioni 150 za Tanzania). Ochan anakuwa mchezaji wa pili wa simba kuuzwa katika mwaka huu, baada ya Mbwana Samata kuuzwa TP Mazembe kwa kitita cha dola 100,000 za kimarekani.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage alisema jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Ochan aliuzwa juzi kwa klabu ya Mazembe na mkataba wake unafana na wa Mbwana Samatta aliyeuzwa kwa Mazembe mwezi uliopita, ambapo wachezaji hao watakuwa wakilipwa mshahara wa dola za Marekani 5,000 ( Sh milioni 7.5) kwa mwezi.
Pia katika mkataba huo klabu ya Simba itakuwa ikipata asilimia 20 ya malipo endapo wachezaji hao watauzwa kwa klabu nyingine na TP Mazembe.
Mbwana Samata amesaini mkataba wa kuitumikia TP Mazembe kwa miaka 3 ambapo atakuwa akilipwa dola za marekani 5,000 sawa na Tsh mil 7.5 kwa mwezi, huku akiwa amekatiwa bima. Malipo hayo ni mbali ya marupurupu mengine ambayo atapatiwa ambayo yanaweza kufikia kiasi cha Sh milioni 90 mwaka.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment