CAF

Okwi aipaisha Simba Setif


Goli la mshambuliaji toka Uganda anae kipiga kwa vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba SC, Emmanuel Okwi limetosha kuipeleka Simba SC katika raundi ya 3 ya kombe la shirikisho CAF, kwa matokeo ya jumla ya goli 3-3. Simba wakivuka kwa faida ya goli la ugenini.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa may 8 mjini Setif, Simba waliuwanza mchezo huo kwa pigo, baada ya beki wao tegemeo Juma Nyosso kuzawadiwa kadi nyekundu katika dakika ya 13 ya mchezo.

ES Setif waliandika goli lake la kwanza katika dakika ya 34 kupitia kwa mshambuliaji wa timu hiyo Mohammed Aoudia mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikuwa mwiba kwa Simba SC.

Aoudia alirejea kwenye nyavu za Simba mara tu baada ya kipindi cha pili kuanza katika dakika ya 46 kabla ya Benmoussa kuhitimisha kalamu ya magoli kwa upande wa ES Setif katika dakika ya 52 ya mchezo.

Juma Kaseja alifanya kazi ya ziada katika dakika ya 65 kwa kuokoa mchomo wa waarabu na mpira kuwa kona tasa, wakati Victor Costa akitokea benchi nusura awapatie goli jingine ES Setif.

Alikuwa Emmanuel Okwi aliyewanyamazisha waarabu katika dakika ya 90 kwa kuipatia Simba SC goli pekee katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kufungwa goli 3-1 na kupelekea matokeo ya jumla kuwa 3-3 baada ya mchezo wa awali wa Taifa kumalizika kwa Simba kuichapa goli 2-0 ES Setif, kwa mantiki hiyo Simba wanapita kwa faida ya goli la ugenini walilopata leo.

Kwa matokeo hayo Simba itakutana na mshindi kati Al ahly shandy ya Sudan na Ferroviaro de Maputo ya Msumbiji, ambapo mchezo wa awali uliopigwa Maputo Msumbiji Ferroviaro de Maputo walifunga goli 1-0.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.