mingine

Dar Swim Club mabingwa washinda mashinano ya kuogelea ya Taliss


Timu ya Dar Swim Club (DSC) imeshinda mashindano ya kuogelea ya Taliss baada ya kuzipiku klabu nyingine nane zilizoshiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule yaKimataifa ya Upanga.

Dar Swim Club  ilijikusanyia pointi 2,421 katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu za wanawake na wanaume.

Katika mashindano hayo, wanawake wa DSC walikusanya jumla ya pointi 1,526 huku wanaume wakijikusanyia pointu 895 kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa.

Waogelaji wa kike Smriti Gokarn, Celina Itatiro na Maia Tumiotto walichangia zaidi ushindi wa timu hiyo kwa kukusanya pointi nyingi na akwa upande wa wavulanai walikuwa Matt Golembeski, Marin De Villard na Carter Golembeski.

Nafasi ya pili ilinyakuliwa na wenyeji Taliss kwa kupata jumla ya pointi 2,298 huu waogelaji wao wa kiume, Adil Dharmal na Oliver Mclntosh wakiongoza kwa kuchangia pointi nyingi katika ushindi huo.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Shule ya Kimataifa ya Moshi ambayo ilichanganyika nay a Arusha kwa kupata pointi 1,111 huku waogeleaji wake, Josephine Oosterhuis na Pieter De Raadt wakichangia pointi nyingi.

Timu ya kuoglea ya Mwanza ilimaliza katika nafasi ya nne chini ya waogeleaji nyota Elia Imhoff na Emma Imhoff  na kufuatiwa ma shule ya kimataifa ya Morogoro chini ya nyota wake, Dennis Mhini na Charlotte Sanford.
wachezaji na makocha wa timu ya Dar Swim Club wakishangilia baada ya kutwaa ushindi wa jumla katika mashindano ya kuogelea ya Taliss yaliyofanyika leo kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya Tangangika (IST Upanga) na kushirikisha jumla ya timu tisa.

Timu ya Bluefins ilishika nafasi ya sita kwa pointi  553 ambapo waogelaji wake Sahal Harunani alishinda medali ya shaba. Nafasi ya saba ilikwenda kwa timu ya Wahoo iliyokuwa chini ya Ellis Underson na Rania Karume kwa kupata pointi 303 na huku Champions Rise na Kennedy House wakimaliza katika nafasi mbili za mwisho.

Mhasisi wa Dar Swim Club Ferick Kalengela alisema kuwa siri kubwa ya ushindi wao ni kujituma na kufanya mazoezi ya kisasa huku Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro akiwapongeza wachezaji wake na kusema huo ni mwanzo tu na makubwa yatafuatia katika kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.