kitaa

KITAANI: TAFAKARI JUU YA TUNUKU YA SERIKALI KWA SAMATTA

Caption ya post ya Fredy Nyanda kutoka katika kundi la Kandanda ndani ya Facebook
Na Fredy Nyanda, Kandanda (Facebook)

Mwaka 2010 pale airport ya buenos Aires Argentina wakati wa mapumziko ya x mass Messi alienda kwao argentina aliposhuka airport alipokelewa na mate usoni wakati akijifuta akapewa na kofi juu aliyempiga kofi ni mwandishi wa habari ambaye alisema messi anaidharau argentina maana hamna cha maana anachokifanya ila akiwa barca anajituma sana baada ya hapo messi alianza kujielewa leo messi anaifukuzia rekodi ya armando diego maradona messi.

Huko bongo mbwana samata amepewa kiwanja pesa na kitambaa cha unahodha juu tujiulize sammata Ameifanyia nini Tanzania???

Ngoja tuone
1)Idadi ya magoli ya sammata timu ya taifa(kwenye mechi za kalenda ya fifa) hayazidi 10

2)Huyu dogo alikua na tabia ya kudodge timu ya taifa kwa njia ya kufodge injury au akija basi akiguswa kidogo usoni anashika ankle ili atoke maana kesho kutwa yake Tp mazembe anacheza na dc motema pembe hivyo hataki kuikosa game hiyo

Sasa amepewa hayo aliyopewa kwa sababu ya tuzo
Tujiulize kwa nini kapewa tuzo hiyo?

Jibu ni kwamba kapewa tuzo hiyo kwa kuipa mafanikio Tp mazembe na sio Tanzania leo wanataka hadi kumpa barabara na kiwanja alichocheza hahahhahaha hivi tukitaja mzalendo wa timu ya Taifa kuna anaemfikia shadrack nsajigwa nafyatufyake?

Wakati sammata amechubuka kidogo anaomba substitues nsajigwa goti kategua mkono wa kushoto kategua na malaria juu kichwa kinamuuma Maximo anamuita bench nsajigwa anakataa maana anajua anawakilisha taifa lake

Wapo wazalendo wengi tu leo hii hawathaminiwi anakuja kuthaminiwa mchezaji wa tp mazembe

Familia ya said mziray mmeithamini??

Marehemu syllivester mash mmethamini mchango wake kivipi?

A VERY PAINFUL DRAMA DONE BY TFF AND THE GOVT
Mwenye kuelewa aelewe.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.