zanzibar

KAMATI ZFA YANG'OLEWA, MAKAMU WA RAISI AONDOLEWA


MKUTANO Mkuu wa dharura wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), umeiondoa Kamati ya Muda ya chama hicho, huku pia ikimuondoa madarakani Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Haji Ameir Haji.

Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano huo uliofanyika jana mjini hapa chini ya Mwenyekiti wa chama hicho Ravia Idarous.

Akisoma maazimio ya mkutano huo, Makamu wa Rais wa ZFA, Pemba, Ali Mohammed alisema uamuzi wa kumuondoa Haji Ameir ulifikiwa kwa kura za ndiyo za wajumbe 43 kati ya 47 waliohudhuria mkutano huo.

Licha ya kuondolewa katika wadhifa huo, pia Makamu huyo wa Rais amefungiwa asijihusishe na soka kwa miaka minne akidaiwa kukiuka katiba ya ZFA kwa kupeleka masuala ya soka mahakamani.

Alisema pia mkutano huo umeiondosha Kamati ya Muda ya ZFA Taifa iliyokuwa ikisimamia masuala ya mpira kwa kukiuka katiba ya chama hicho kwani masuala ya mpira yanasimamiwa na Kamati ya Utendaji.

Chanzo: Habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.