CAF

JKU WACHAPWA 4 NA SC VILLA


Wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya kombe la shirikisho la CAF JKU wametanguliza mguu mmoja nnje baada ya kukubali kichapo cha goli 4-0 kutoka kwa SC Villa ya Uganda mchezo uliochezwa nchini Uganda.

Katika mchezo huo wa leo JKU walienda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli 2-0 kabla ya kipindi cha pili kuruhusu magoli mengine 2 na kupeleka mchezo kumalizika kwa SC Villa wakiibuka na ushindi wa goli 4-0.

Kwa matokeo ya leo inawalazimu JKU kusaka ushindi wa goli zaidi ya 5 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa katika mchezo wa marejeano itakayofanyika mwishoni mwajuma lijalo katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.