CAF

JKU WATOLEWA NA SC VILLA KWA GOLI 5-0

Makamu bingwa wa ligi kuu ya Uganda SC Villa imefanikiwa kuwaondosha makamu bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar JKU katika michuano ya kombe la shirikiso la soka Afrika CAF.

JKU imeondolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya magoli 5-0 baada ya leo kukubali kichapo cha goli 1-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Amani.

Katika mchezo huo ambao JKU walicheza vyema kulinganisha na mchezo wa awali uliochezwa jijini Kampala ulishuhudia dakika 45 zikimalizka wakiwa sare ya bila kufungana.

Katiki dakika ya 46 SC vilaa waliandika goli pekee katika mchezo huo kupitia kwa Ambroice na kupeleka mchezo kumalizka kwa SC Villa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.