ZGPL

CHIPUKIZI, MWENGE ZAENDELEA KUTAMBA LIGI KUU ZANZIBAR


Kindumbwendumbwe cha ligi kuu ya Zanzibar kimeendelea tena leo kwenye uwanja wa Gombani na FFU Finya majira ya alasiri.

Katika mchezo wa Gombani kati ya African Kivumb i ya Mwambe na Chipukizi ya Chake Chake, A/Kivumbi imejikuta ikalala mbele ya wakongwe hao kwa mabao 2-0.

Mchezo ulianza na kasi kwa temu zote kuonyesha umahiri wao wa kupiga pasi maridadi, lakini hadi lakikaa 45 za kipindi cha kwanza kinakwisha hakukuwa na mbabe aliyeweza kuziona nyavu za mwenzake.

Katika dakika ya 37 ya mchezo walimpumzisha Samir Ali Simai na nafasi yake kuchukuliwa na Abdul-karim Ali, huku mwanzoni mwa kipindi cha pili A/Kivumbi waliwatoa nje Fred Ramos na Ibrahim Abdalla na kuwaingiza Zakaria Bakari na Ali Mussa.

Bao la kwanza la Chipukizi limefungwa na mchezaji Abdul-karim Ali aliyetokea bench baada ya kuutumbukiza wavuni kwa urahisi mpira uliokoswa na mlinzi wa A/Kivumbi Mustafa Moh`d katika dakika ya 65.

Alikuwa Abdul-Karim Ali kwa mara ya pili aliyewanyanyua mashabiki wa Chipukizi kwa kuanzika bao safi katika dakika ya 88.

Na hadi mwisho wa mchezo huo Chipukizi 2 na African Kivumbi hawakupata kitu.

Chipukizi tayari imeshashinda michezo yake yote mitatu iliyocheza huku kwa A/Kivumbi akishinda mmoja,kutoka sare 1 na kufungwa mmoja.

Na huko kwenye uwanja wa FFU Finya Mwenge wakaisambaratisha Sharp Victor kwa jumla ya magoli 2-0.

Kesho kutakuwa na michezo miwili pia,uwanja wa Gombani Madungu watawakaribisha Aljazira na FFU Finya Okapi watavaana na Kizimbani.

Chanzo: Salma Sport's Media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.