ZGPL

IDUMU YAWA YA KWANZA KUSHUKA DARAJA


Idumu imekuwa ndio timu ya mwanzo kuondolewa katika kinyang’anyiro cha kucheza ligi kuu ya Zanzibar baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Chwaka, katika mchezo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani hapa mjini Unguja.

Timu ya Chwaka jana imemaliza michezo yake yote ya hatua ya sita bora kanda ya Unguja na kufanikiwa kuwa vinara wa  ligi daraja la kwanza taifa ikiwa na alama 11, kwani alama hizo hakuna timu yoyote itakazo zifikia katika ligi hiyo.

Chwaka walianza kupata mabao ya mapema, ambapo mchezaji Awadh Salum ameweka mabao mawili katika dakika ya 4, na dakika ya 12, na mnamo dakika ya 29, Suleiman Omar akaipatia Chwaka bao la tatu.

Kipindi cha pili Chwaka walionekana kujisahau kabisa na kuridhika na mabao waliyoyapata, ndipo Idumu wakaanza kuja kwa kasi, na ndipo Othman Khamis akaipatia Idumu bao la kwanza, na katika dakika ya 80 Idumu wakapata bao la pili lililofungwa na Khamis Haji.

Na mtanange huo ulimalizika kwa Chwaka kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, na kuwaondoa Idumu katika kinyang’anyiro cha kucheza ligi  kuu ya Zanzibar msimu ujao wa mwaka 2016 – 2017.

Idumu wamemaliza michezo yote huku wakiondoshwa katika kinyang’anyiro hicho cha ligi kuu wakiwa na alama nne 4, na Chwaka wamemaliza michezo yake wakiwa ndio vinara na alama 11, huku wakisubiri kucheza ligi kuu msimu ujao wa mwaka 2016 – 2017.

Chanzo: Salma Spotrs Media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.