ZGPL

JKU YAENDELEZA UBABE LIGI KUU YA ZANZIBAR


Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU), imezidi kujikita kileleni mwa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya leo kuibuka na ushindi walipocheza na Kijichi.

Katika mchezo huo uliochezwa ndani ya uwanja wa Amani, JKU walifanikiwa kuifunga timu ya Kijichi kupitia mchezaji wake Emmanuel Martin katika dakika ya 49 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa  Khamis Abdalla Terry.

Akizungumza na SALMA SPORTS MEDIA kocha wa timu ya Kijichi Abdul Kiduu amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri,” mchezo ulikuwa mzuri, timu imecheza vizuri lakini marifa wajitahidi, mchezaji ata akifanya vibaya rifa hatowi, timu yetu inahakika hata kwenye nne itaingia kwa sababu inaperform vizuri, ispokuwa mambo madogomadogo tu, naamini game ijayo watu wataona ushindi”. Alisema kocha Kiduu.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa timu ya JKU Khamis Muhsin nae amesema kwamba wamejipanga kwa mechi inayofuata,” tumejipanga kwa mechi inayofuata, ushindi unashangiria ushindi wowote tu kwa hiyo point tatu tu mezipata sie bado tunasonga mbele”. Alisema kocha Khamis.

Timu ya Kijichi licha ya kucheza vyema dhidi ya JKU katika mchezo huo lakini walishindwa kupata bao lolote na mchezo huo ulimalizika kwa JKU kuibuka na ushindi na kuzidi kujiweka kileleni mwa ligi hiyo.

Matokeo hayo yameifanya timu ya JKU kufikisha alama 41 wakiwa ndio vinara wa ligi hiyo, na Kijichi wao wapo nafasi ya 12 na alama 14.

Chanzo: Salma Sports Media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.