ZGPL

JKU YAENDELEZA UBABE LIGI KUU ZANZIBAR, YAICHAPA JANG'OMBE


Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) imeendelea kuonesha ubabe wake na kuzidi kujiweka kileleni mwa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja bada ya kuwabamiza Jang’ombe boys mabao 2-1.

Katika mtanange huo uliochezwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za Jioni JKU walianza kupachika bao katika dkk ya 36 lililofungwa na Moh’d Abdallah.

Na bao la pili lilifungwa na Emmanuel Martin mnamo dakika ya 46 ya mchezo huo.

Kwa upande wa Jang’ombe boys bao la kufutia machozi limewekwa kimyani na Bakar Thani katika dkk za nyongeza za mchezo huo.

katika mchezo huo mchezaji wa JKU Khamis Said ameoneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Jang’ombe boys Juma Ramadhan.

Akizungumza na SALMA SPORTS MEDIA kocha wa timu ya Jang’ombe boys Issa Othman Amasha amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri kwa timu zote mbili, “mchezo ulikuwa ni mzuri kwa timu zote mbili ila JKU wameonesha uzoefu katika mchezo wa leo, tumefungwa kwa sababu JKU ni wazoefu kuliko wachezaji wangu kwa sababu ni bado wadogo na ni msimu wa kwanza kuja ligi kuu”.

Aidha Amasha aliendelea kusema,

“Tamaa ya kuelekea nne bora sasa haipo ila tujitahidi tubakie daraja tu kwa sababu mechi tunapoteza tu pint tunazo kidogo kuna watu wana point 28, 30 sasa kwa mm siwezi ninaejua mpira siwezi kusema nina tama ya kuingia nne bora wakati tuna point 18, jitihada tutaonesha kuhakikisha timu yetu inabakia daraja”.

Pia kocha msaidizi wa JKU Khamis  Muhsin nae amesema “mchezo ulikuwa mzuri ila kutokana na viporo vya apo kwa apo tumecheza juzi tumekuja na leo tunacheza na kesho kutwa tunacheza tena na ndio maana unawakuta wachezaji wapo chinio kidogo”.

Kwa matokeo hayo JKU imezidi kujiweka kileleni wakiwa na alama 38, na Jang’ombe boys wakiwa nafasi ya 11 na 18.

Chanzo: salama Sports Media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.