ZGPL

YOUNG ISLANDER YAZINDUKA KWA MADUNGU NA KUICHAPA 3


Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Zanzibar dhidi ya African Kivumbi timu ya Young Islander jana ilifuta makosa yake kwa kuibamiza timu ya Madungu kwa jumla ya magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Gombani.

Katika mchezo huo ambao watazamaji hawakuwa wengi Young Islanders walianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 35 kupitia kwa mchezaji wake Fahdi Ali, huku la pili likifingwa na Amour Issa kwenye dakika ya 44.

Na hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Young Islanders walikuwa wanaongoza kwa magoli 2-0.

Kuanza kipindi cha pili Madungu walionekana kuja juu jambo lililopelekea kujipatia bao kwenye dakika ya 55 lilifingwa na mchezaji wake Kassim Juma ambaye aliingia akitokea benchi.

Dakika 2 kabla ya kumalizika kwa mchezo huo Fahdi Ali wa Young Islanders aliiaandikia timu yake goli la 3.

Hadi dakika 90 za mwamuzi Hassan Gerei zinamalizika Young Islanders 3 na Madungu 1.

Na katika mchezo mwenye wa ligi kuu ya Zanzibar Kanda ya Pemba uliochezwa jana katika uwanja wa FFU Finya timu ya Shaba ya Kojani imeendeleza ubabe kwa kuicharaza Okapi ya Msuka kwa jumla ya mabao 3-1.

Leo kutakuwa na michezo miwili, kwenye uwanja wa Gombani Chipukizi wataikaribisha African Kivumbu na FFU Finya Mwenye watakuwa uso kwa uso na Sharp Victor.

Chanzo: Salma Sports Media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.