ZGPL

JKU YAVUTWA SHATI

Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU, leo imelala baada ya kufungwa goli 1-0 kutoka kwa Zimamoto katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.

JKU leo hawakuonesha kabisa kiwango chao na wamecheza tofauti na walivyozoeleka, pia walikosa nafasi za kufunga na kuwapa mwanya timu ya Zimamoto ambao walijipatia bao pekee.

Zimamoto wamepata bao hilo kupitia mchezaji Amour Juma alilolifunga katika dakika ya 38.

JKU ni mchezo wake wa tatu sasa kuupoteza katika mechi 20 walizocheza, tangu kuanza kwa ligi amabpo wamepoteza walipokutana na Black sailor 1-0, pia wamepoteza kwa Miembeni 1-0, na leo wamefungwa na Zimamoto 1-0.

Zimamoto sasa wamepanda hadi nafasi ya pili wakiwa na alama 35 katika msimamo wa ligi hiyo,na JKU licha ya kuupoteza mchezo huo lakini bado wanaongoza ligi wakiwa na alama 47.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.