ZGPL

KMKM WACHARAZWA 3-2 LIGI KUU ZANZIBAR.

Mabaharia wa KMKM wamepata kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Kimbunga katika mchezo wa ligi kuu ya zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa maira ya saa kumi za jioni ndani ya dimba la Amani.

Katika mtanange huo Ali Tunu alianza kuiandikia Kimbunga bao la kuongoza katika dakika ya 44,na timu hizo zilikenda mapumziko Kimbunga wakiwa mbele kwa bao 1-0.

KMKM wakafunga bao la kusawazisha lililowekwa kambani na mchezaji Amour Ali katika dakika ya 49, ambae alitokea bench na kuchukua nafasi ya Haji Simba.

Mnamo dakika ya 66 KMKM wakapata bao la pili nalo lilifungwa na mchezaji aliyetokea bench Nassor Ali, aliyechukua nafasi ya Faki Mwalim.

Mtanange huo ulizidi kuwa wa kasi na Kimbunga wakasawazisha bao la pili liliwekwa kimyani na Waziri Ramadhan mnamo dakika ya 75, na Ali Tunu akarudi tena nyavuni kwa kuipatia Kimbunga bao la ushindi katika dakika ya 88 ya mtanange huo.

Matokeo hayo yameifikishia Kimbunga alama 26, na nafasi ya tisa 9, na KMKM wapo nafasi ya nne 4 alama 33 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Chanzo: SALMA SPORTS MEDIA

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.