ZGPL

MTENDE WAENDELEA KUPOTEA, WAKUBALI KICHAPO CHA GOLI 2


Timu ya Mtende rangers imezidi kuyumba katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kuchezea  kichapo cha mabao 2-0 walipocheza na mabaharia weusi timu ya Black sailors katika mchezo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani mjini Unguja.

Mabao ya Black sailors yamefungwa na Mustafa Vuai katika dakika ya 27, na Abdul-Aziz Hassan dakika 37.

Mtende walionesha kiwango kizuri na wameweza kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa lakini walikosa mabao mengi katika mtanange huo, licha ya kucheza vyema lakini Mtende walimaliza mchezo bila ya mafanikio yoyote, kwa kufungwa kwa mabao 2-0.

Mtende bado wanaburuta mkia wakiwa na alama kumi 10, na Black sailors wao wapo nafasi ya saba 7 na alama 29.

Chanzo: Salma Sports Media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.