ZGPL

POLISI WACHEZEA KICHAPO KWA ZIMAMOTO


Timu ya Polisi bado ipo katika wakati mbaya katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya leo kuupoteza mchezo wake walipocheza na Zimamoto kwa kucharazwa mabao 2-0.

Katika mchezo huo uliosukumwa majira ya saa kumi za jioni ndani ya dimba la Amani, mabao ya Zimamoto yamewekwa kambani na Hakiim Khamis katika dakika ya 43 na 64.

Polisi wameshinda mchezo mmoja tu tangu kuanza kwa ligi hiyo katika michezo takriban 19 waliyocheza na sasa wana alama 10 katika msimamo wa ligi hiyo.

Zimamoto wao wapo nafasi ya tatu 3 wakiwa na alama 32 katika msimamo wa ligi hiyo.

Chanzo: salma sports media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.