mtazamo

PPKAHEMELA SAHIHI TULIZOEA KUIONA KATIKA WEBSITE YA AZAM FC, AMBAYO IMEHAMIA SIMBA

Katibu Mkuu Mpya wa Simba SC Patreck Kahemela
Kuna maeneo mengi ambapo soka letu la bongo limevipuuza na moja ya eneo ni lautoaji taarifa muhimu kwa wadau wa soka nchini, kutoka kwa wa husika wa hizo habari.

Ukitaka taarifa yoyote kuhusiana na soka letu, inakubidi ungoje vipindi vya michezo vya redio, runinga, magazeti ama katika mitandao yetu ya michezo, ambapo ukiondoa runinga na redio ambao ni ngumu kusikia ama kuona taarifa ambayo si rasmi kutoka sehemu husika (Vilabu ama shirikisho la soka).

Kwa miaka ya 8 ya klabu ya Azam FC imejizoeleea umaarufu katika upande wa mitandao na kupata wafuasi wengi katika kurasa yao rasmi ambapo kwa ndio inaongoza ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati, na yote hayo yalikuwa yanafanywa nyuma ya pazia na meneja Mpya wa Simba SC Patrick Kahemela.

Kuondoka kwa Kahemela ndani ya Azam FC na kujiunga na Simba SC ninahamu sana kuiona Azam FC inatakavyoendelea kudumisha utamduni wao wa kuwataarifu umma kupitia mitandao yao ya kijamii na website yao, vile vile nikingoja maisha mapya ya Simba SC katika mitandao.

Kahemela ni miongoni mwa watu wachache katika soka letu ninao wahusudu, nani matumaini yangu viongozi wa simba sc watamtumia vizuri, nakama vigisu zetu za soka zikiendelea sitoshangaa kuona ama kusikia Kahemela kushindwa kumudu Simba SC angalau Mwaka Mmoja.

Ili malengo ya Kahemela yatimie ndani ya Simba SC kunahitajika kuwepo kwa ushirikiano baina ya mashabiki, wanachama na viongozi wa simba sc, na endapo kukikosekana ushirikiano sidhani kama kunajambo jipya atakalo lileta ndani ya Simba SC.

Nitaimisi signetare hii ppkahemele katika website ya Azam FC na nimeguswa imbasavyo kwa kazi yako nzuri uliyoifanya ukiwa Azam FC na nina kutakia kila la kheri.

Imeandikwa na Abdallah H.I Sulayman
Shabiki na msimamizi wa blog ya Chama langu ni Azam

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.