VPL

SINGIDA, YANGA YATENGENEZA MAZINGIRA YA SIMBA SC KUREJEA KILELENI

Matokeo ya sare katika kiwanja cha uhuru na Jamuhuri ambapo wenyeji wa michezo hiyo walikuwa ni Yanga na Singida United yametengeza mazingira ya Simba SC yenye pointi 8 kurejea kileleni hapo kesho kama watashinda mchezo wao dhidi ya Stand united.

Yanga wametoka sare bila ya kufungana na vinara wa ligi kuu Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru huku Azam FC waliopo nafasi ya pili wakiokolewa na kinda wa kikosi B Paul aliyeisawazishia timu hiyo katika dakika ya 87 na kupelekea kuambulia sare ya goli 1-1 mbele ya Singida united, mchezo uliochezwa katika uwanja wa jamuhuri mkoani Dodoma.

Katika michezo 7 ya ligi kuu hii leo michezo 6 imeisha kwa sare huku Ndanda Fc wakiwa timu pekee iliyoibuka na ushindi wa goli 2-1.

Simba SC kesho atakuwa katika uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kuikabili Stand united na endapo wakishinda watafikisha pointi 11 sawa na Mtibwa na Azam ila Simba anawazidi Mtibwa na Azam idadi ya magoli ya kufunga hivyo kuwafanya kukaa kileeni.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.