VPL

NJOMBE YA ICHAPA RUVU SHOOTING

Kikosi cha Njombe Mji
Timu ya Njombe Mji hii leo wamefanikiwa kuvuna pointi tatu mbele ya Ruvu shooting ya Pwani katika mwendelezo wa ligi kuu ya vodacom iliyo fikia mzunguko wa 20.

Katika mchezo huo wa leo ulioanzaa saa nane mchana katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Njombe Mji ndio walikuwa wa mwanzo kuona nyavu za Ruvu shooting katika dakika ya 27 kupitita kwa Ditram Nchimbi, goli lililo dumu kwa dakika 5, ambapo Ruvu shooting walisawazisha kupitia kwa Baraka Mtuwi.

Njombe Mji walipata goli lao la ushindi katika dakika ya 56 kupitia kwa Jimmy Mwasondola na kuwafanya kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Kwa matokeo hayo Njombe Mji anafikisha pointi 18 akiwa sawa na Ndanda FC, huku wakiziacha Kagera Sugar na Majimaji wakiwa mkiani kwa kuwa na pointi 15 ambapo hii leo wanacheza.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.