vilabu

MBEYA CITY KAMILI YAELEKEA SHINYANGA KUFUNGUA LIGI

BAADA ya mazoezi ya majuma kadhaa pamoja na michezo ya kirafiki, kikosi cha Mbeya City Fc kinataraji kuondoka jijini Mbeya kesho asubuhi kuelekea mkoani Shinyanga, tayari kwa mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara  dhidi ya wenyeji Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera.

Afisa habari, Dismas Ten ameiambia mbeyacityfc.com kuwa,City inaondoka jijini Mbeya kuifuata Kagera Sugar ikiwa na  kikosi cha wachezaji 22 sambamba na  viongozi 9 tayari kwa mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya,uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kufuatia uwanja wa Kaitaba  mjini buko kuwa bado kwenye matengenezo.

“Ni kikosi cha wachezaji 22 pamoja na viongozi 9, wanasafiri kuelekea  Shinyanga tayari kwa mchezo huo wa kwanza,kwetu sisi huu ni mchezo muhimu katika mipango na mikakati yetu ya kuhakikisha  tunafanya  vyema msimu huu, kila mmoja anafahamu ubora wa timu yetu, tangu tumepanda daraja  tumekuwa sehemu ya mapinduzi katika soka la nchi yetu,”alisema.

Akiendelea  zaidi  Ten alisema kuwa kwenye iadidi hiyo ya  wachezaji 22 wamo pia wachezaji wote waliojumuishwa kikosini  katika usajili  uliopita ambao watakuwa wanapewa nguvu na ushirikino kutoka kwa wachezaji waliokuwepo ndani ya kikosi katika msimu uliopita.

Miongoni mwa wachezaji walisafiri ni pamoja na mlinda mlango chipukizi Hamis Msabila ambaye  amekuwa akionyesha uwezo mkubwa tangu alipopandishwa kikosi akitokea U20. wengine ni pamoja na Medson Mwakatundu,Michael Kerenge,Hassan Mwasapili,Ditram Nchimbi,Peter Mwangosi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.