vilabu

Moro united kuitwa Tabata fc

aamsuni
Timu ya moro united ya jijini Dar es salaam ipo katika mchakato wa kubadili jini. Mwenyekiti wa klabu Redgers Peter amesema "wadau mbalimbali Tabata tumeipandisha daraja timu yetu na tunachotaka ni kuibadilisha jina kuwa Tabata Fc na tayari tumekwisha anza mchakato".
Moro united hapo awali maskani yake ilikuwa Morogoro, kabla ya Kassim Dewij kuinunua na kuiamishia Dar es salaam. Moro united ni miongoni mwa klabu chache nchini zilizo shuhudia kumilikiwa na watu tofauti, katika vipindi tofauti, na pia kubadilishwa kwa jina lake.
Moro united iliyorejea ligi kuu, baada ya kushuka daraja katika msimu 2009/2010, imeanza kujipanga kwa ligi kuu msimu ujao. Timu nyingine zilizopanda kwa ajili ya msimu 2011/2012 ni coastal union ya Tanga, Villa Squard ya Dar es salaam, pamoja na Jkt oljoro ya Arusha.
Moro united wameanza kufanya mazungumzo na baadhi ya nyota wa simba na yanga ambao ni, Meshack Abel, Amir Maftah, Jerry Tegete, Nurdin Bakari na Halfan Razaki. Hayo yamethibitishwa na mwenyeketi Redgers Peter kuwa wameanza mazaungumzo ya awali, na lengo ni kuwa na timu yenye ushindani ligi kuu.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.