CAF

OKWI NA BOCCO FITI KUWAVAA WARABU, MCHEZO KUCHEZWA USIKU, VIINFILIO VYATAJWA

Nahodha wa Simba SC John Bocco na mshambuliaji wa timu hiyo Emanuel Okwi wako fiti kucheza mchezo wa kombe la shirikisho la soka Afrika, dhidi ya Al-Masry ya nchini Misri, mchezo utakaochezwa jumatano wiki hii katika uwanja wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, afisa habari wa Simba SC Haji Manara amesema kuwa wachezaji hao waliokosekana katika mchezo wa jana dhidi ya Stand United wako fiti kucheza katika mchezo wa shirikisho siku ya jumatano.

Manara akizungumzia maandalizi ya mchezo huo amesema kuwa mchezo huo utaanza saa 12 jioni badal ya saa 10 alasiri na tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho kutwa (jumatatu).

“Tumeweka viingilio vya aina tatu, mzunguko pamoja na Orange kiingilio itakuwa ni Tsh. 5000, VIP B Tsh. 15,000 na VIP A Tsh. 20,000. Kuanzia keshokutwa vituo vyote vya Puma na sehemu nyingine zote ambazo nitazitaja kesho zitauzwa tiketi na watu wa Selcom kama ilivyo dasturi. Tutajitahidi kuwe na centre nyingi ili watu wapate tiketi kwa urahisi.” alise Manara.

“Klabu ya Al Masry itawasili kesho (Jumapili) jioni saa 12, siku ya Jumatatu jioni wafanya mazoezi kwenye uwanja wa taifa kama kanuni zinavyotaka kwa sababu Jumanne kutakuwa na mchezo wa klabu bingwa kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers.”

“Waamuzi watawasili siku ya Jumatatu saa 10 jioni kutoka Afrika Kusini lakini mechi kamishna anatoka Elitrea ambaye atawasili siku moja pamoja na waamuzi.”

“Pre-match meeting itafanyika siku ya Jumanne jioni kwenye hotel ya Golden Tulip. Maandalizi mengine ndani ya timu yetu yanakwenda vizuri, timu imeingia kambini leo baada ya mchezo wa jana wa ligi kuu."

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.