CAF

AL-MASRY WAAMBULIA SARE KWA SIMBA, PENATI TATU ZAPIGWA

Mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Simba SC na Al-masri ya Misri umemealizika kwa sare ya goli 2-2, huku kukishihudia kutolewa kwa penati 3 na mchezo kusimama baada ya taa kuzimika.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Hando Helpus akisaidiwa na Zakjele Thusi na Athenkosi Ndongeni wote kutoka Afrika Kusini, ulibidi usimame latika dakika ya 84 baada ya taa za uwanja wa Taifa kuzimika, na ulisimama kwa takribani dakika 30 kabla ya ku,alizia dakika 6 zilizo kuwa zimesalia.

Simba SC walikuwa wa kwanza kupata goli kwa mkwaju wa penati uliopigwa na John Bocco katika dakika ya 9 ya mchezo, penati hiyo ilitokana na mchezaji wa Al-masry kuushika mpira katika eneo la hatari.

Katika dakika 11 ya mchezo Al-masri walisawazisha goli hilo kupitia kwa Ahmed Goma aliounga krosi kutoka upande wa kushoto wa uwanja.

Iliwachukuwa dakika 15 Al-masry kuziona nyavu za Aish Manula kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Ahmed Abdalraof, penati iliyotokana na James Kotei kuushika mpira katika eneo la hatari na kupeleka timu hizo kwenda mapumziko Al-masry wakiwa mbele kwa goli 2-1.

Kipindi cha pili Simba SC walifanya mabadiliko ya kumtoa Yusufu Mlipili na nafasi yake ikachukuliwa na Said Ndemla katika dakika ya 71, huku John Bocco akimpisha Laudit Mavugo katika dakika ya 61.

Mabadiliko hayo yaliimarisha Simba SC katika eneo la kati na kupelekea kupeleka mashambulizi ambapo katika dakika ya 73 walipata penati na Emanuel Okwi kuifungia Simba SC goli la pili.

Wakati Simba SC wakizidisha mashambulizi ya kusaka goli la tatu, katika dakika ya 83 umeme ukazimika uwanja wa taifa huku mvua kubwa ikiwa inanywesha kitendo kilichopelekea baadhi ya mashabiki kudhani huenda mchezo ukashindwa kumalizika hii leo.

Baada ya dakika takribani 30 mchezo uliendelea na kumalizika kwa sare ya goli 2-2 na kuifanya Simba SC kuhitaji ushindi waina yoyote ule ama sare ya kuanzia goli 3-3 ili wa weze kufuzu kwa hatua ya mwisho kabla ya hatua ya makundi.

Kikosi cha Simba SC; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, James Kotei, Yusufu Mlipili/Said Ndemla dk71, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya na John Bocco/Laudit Mavugo dk61.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.