aamsuni
Timu ya taifa chini ya miaka 23 'vijana stars' wataondoka leo kuelekea Cameroon kwa ndege ya Kenya airways. Vijana stars watawavaa Cameroon siku ya jumapili ya tarehe 27 mwezi huu katika mchezo wa kufuzu kushiriki olimpic mwakani.
Msafara wa timu ya taifa itawausisha wachezaji 19, kocha Jamhuri Kihwelo Julio, kocha msaidizi Ayuob Mohamed, meneja wa timu Mohamed Rashid, daktari wa timu Dr. Joachim Mshanga, mtunza vifaa Edward Evance na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Athuman Kambi ambaye ndio mkuu wa msafara.
Wachezaji wanao ondoka ni Jamal Mnyate, Salum Telela, Omega Seme, Mussa Gharib, Cosmas Lewis, Abdulrahim Shaaban, Zahoro Pazi, Issa Rashid, Himid Mao, Salum Abubakar, Mcha Khamis, Amour Suleiman, Samuel Ngasa, Shomari Kapombe, Babu Ally, Bakari Hamis, Faraji Kabali, Thomas Ulimwengu na Shaaban Hassan.
Kocha Julio amesema kikosi chake kipo teyari kwa ushindani na wanategemea kupata matokeo mazuri mjini Yound, Cameroon.
Nahodha wa timu hiyo Himid Mao amesema wanamatumaini ya kufanya vyema katika mchezo huo, na anaomba dua kwa watanzania ili waweze kufanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment