TFF

Kikosi kitakacho cheza na Taifa stars cha tajwa

aamsuni
Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itakayo kuja nchini kucheza na Taifa Stars, mchezo wa kufuzu mataifa huru Afrika cha tajwa. Msafara wa timu hiyo wenye watu 32 utaongozwa na waziri wa Michezo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Aurelien Zingas.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema kuwa wamepata taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Jamhuri ya Afrika ya Kati ( FCF) kuwa, msafara huo utakuwa na wachezaji 23 ambao ni Prince Samola, Delphin Gbazinon, Audin Boutou, Nicaise Ozingoni, Mamadi Saoudi, Hilaire Momi, Geoffroy Lembet, Euloges Enza, Manasse Enza, Foxi Kette-Vouama, David Manga, Habib Habibou.
Wengine ni Josue Balamandji, Fernander Kassai, Salif Keita, Freddy Lignanzi, Amores Dertin, Eudes Dagoulou, Vianney Mabide, Charly Dopekoulouyen, Emmanuel Yezzouat, Onassis Kemo na Franklin Anzite.
Mchezo utafanyika Uwanja wa Taifa ni wa muhimu kwa Taifa stars ambayo inashika nafasi ya 3 katika kundi lake, huku jamuhuri ya Afrika ya Kati ikiongoza kwa point 4 sawa na Morocco.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.