TFF

Kili Taifa cup kutimua vumbi mei 7

aamsuni

Kili Taifa cup 2011 inatarajiwa kuanza Mei 7, huku hatua ya awali kuanza mwezi ujao. Mwaka huu tofauti na miaka iliyopita, michuano hii itaanzia katika ngazi ya wilaya kutafuta combine ya mkoa, na mchezaji asiyepitia hatua hiyo hato kubaliwa kushiriki michuano hiyo ya mikoa 23 ya Tanzania bara.
Mashindano ya safari hii yameboreshwa katika upate wa zaidi pamoja na sehemu nyingine muhimu. Bingwa mwaka huu atanyakua kitita cha Tsh milioni 40, mshindi wap pili akipata tsh milioni 20, na watatu kuchukua milioni 10.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah alisema “Tunawapongeza TBL kuendelea kudhamini mashindano haya ambayo ni ya kihistoria, kwani wanagharamia mambo mengi, ikiwamo nauli za timu shiriki, vifaa hadi zawadi za ushindi. Lakini udhamini huu haumaanishi mikoa kutegemea TBL pekee, bali wauboreshe udhamini huu, mikoani kuna hoteli, makampuni na taasisi mbalimbali, mikoani ni kila kitu, hivyo viongozi waanze sasa maandalizi ili kuleta ushindani na hatimaye kufanya vizuri katika mashindano haya”.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema huu ni mwaka wa tatu mfululizo kudhamini mashindano hayo, hivyo wanajivunia kufikisha soka ya Tanzania katika kilele cha mafanikio, kutokana na kuzalisha wachezaji kwa ajili ya klabu kubwa hapa nchini.
TBL kupitia kilimanjaro premium lager inataria kutumia tsh milioni 800 katika mashindano ya mwaka huu, ambazo zitatumika kwa ajili ya maandalizi ya timu, usafiri, malazi na vifaa vya michezo.
Zawadi nyingine ni pamoja na mfungaji bora Tsh milioni 2.5, kipa bora, kocha bora, refa bora na mchezaji mwenye nidhamu kila mmoja ataondoka na Tsh milioni mbili huku mchezaji bora wa mchezo atachukua Tsh 100 ,000. Hatua ya mtoano Kili Taifa Cup 2011 itapigwa kwenye vituo sita huku kuanzia hatua ya robo fainali itafanyika Dar es Salaam.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.