TFF

Kuiona Stars na Africa ya kati ni Tsh 3000

aamsuni
Timu ya Taifa, Taifa stars inatarajiwa kushuka uwanjani kuwakabili Jamhuri ya Afrika ya Kati hapo machi 26 mchezo wa kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) kwenye uwanja wa taifa, Dar es salaam.
Viingilio katika mchezo huo ni kama ifuatavyo;
Viti vya Kijani na Bluu Tsh. 3,000
Viti vya Rangi ya Chungwa (Orange straight and curve) Tsh. 5,000
VIP C Tsh. 10,000
VIP B Tsh. 20,000
VIP A Tsh. 40,000

Tiketi zitaanza kuuzwa Machi 24 saa 2 asubuhi katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Big Bon Msimbazi (Kariakoo), Mgahawa wa Steers (Mtaa wa Samora/Ohio), Kituo cha Mafuta OilCom (Ubungo), Uwanja wa Uhuru, Kituo cha Mafuta Kobil (Buguruni) na Kituo Kidogo cha Polisi Tandika Mwisho.
Asilimia moja ya mapato yatakayo patikana katika mchezo huo utatolewa kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha wanachama wake wote ( vyama vya soka vya mikoa pamoja na vilabu) kuwa, hawatambui uongozi wa kupinduliwa kama katiba zao zinavyo eleza. Kwa nafasi zilizowazi zijazwe kwa njia ya uchaguzi.

Pia Tff imekabidhi hundi ya milion 5.2 kwa kila kilabu inayoshiriki ligi kuu ya vodacom msimu 2010/11, ukiwa mgao wa mwisho wa klabu kutoka kwa mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania bara Vodacom.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.