TFF

Mbwana Samatta aenguliwa kikosini

aamsuni

Kocha wa vijana stars, Kiwhelo ametangaza kikosi cha wachezaji 25 na kuwaacha washambuliaji Samatta na Ulimwengu. Mbwana Samatta alisababisha mvutano baina ya kocha Julio na uongozi wa klabu ya simba wa nani mwenye haki ya kumtumia.
Julio amekubali kumwacha nyota huyo pamoja na Ulimwengu aliyetakiwa kufanya majaribio na timu  ya TP Mazembe. "Tumemuacha Samatta kwa sababu klabu yake imeshindwa kumruhusu kujiunga nasi katika kipindi chote cha mazoezi hivyo hatoweza kutusaidi sana kwa sasa ila bado ni miongoni mwa wachezaji wetu," alisema Julio. Akimzungumzia Ulimwengu alisema wamelazimika kumpa ruhusa ili akafanye majaribio yake na TP Mazembe atakapomaliza atarejea kwenye kikosi hicho.
Kikosi hiko kitacheza mechi ya kirafiki zidi ya Azam fc hapo jumatano na ijumaa watacheza na Mtibwa sugar, na kabla ya kwenda Cameroon watacheza na timu ya Uganda ambayo bado aijapangwa itachezewa wapi katika harakati za kujianda kuwakabili Cameroon katika mechi ya kufuzu kushiriki olympic nnchini uingeleza.
Kikosi cha Ngorongoro kinaundwa na Shabani Kado (Mtibwa Sugar), Gharib Mussa (Mtende Rangers), Salum Telela (Yanga), Faraja Kabari (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Mbwana Hamis (Simba), Shomari Kapombe (Polisi Morogoro), Idrisa Juma (KMKM), Abdul Gulam (Malindi), Seme Omega (Yanga), Himid Mao (Azam), Babu Ally (Morani), Ibrahim Rajabu (Azam), Salum Abubakar (Azam), Awadh Juma (Azam), Godfrey Wambura (Simba), Jamal Mnyate (Azam), Frank Domayo (JKT Ruvu), Cosmas Fred (Azam), Mcha Khamis (Zanzibar Ocean View), Ventlaus John (KMKM), Eddo Christopher (Simba), Amour Suleiman (Zanzibar Ocean View), Zahoro Pazi (African Lyon), Samwel Ngasa (African Lyon).

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.