TFF

Mohamed Adolf meneja wa Vijana Stars

aamsuni
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, ambae pia ni mwalimu wa mpira wa miguu kitaaluma, Mohamed Adolf ameteuliwa kuwa Meneja wa timu ya Taifa ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 inayosaka tiketi ya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini London, Uingereza.
Timu hiyo ambayo inafundishwa na Jamhuri Kihwelo akisaidiwa na Mohamed Ayoub itacheza mechi ya mchujo ya michuano hiyo dhidi ya Cameroon. Mechi hiyo ya kwanza itachezwa Machi 27 mwaka huu jijini Yaounde.
Timu hizo zitarudiana jijini Dar es Salaam wiki mbili baadaye.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.