TFF

Nizar, Babi, kuikosa Afrika ya kati

aamsuni

Joto la pambano baina ya Taifa stars na Jamhuri ya Afrika ya Kati imepanda, huku Taifa stars kukosa mashuti ya Nizar na Babi pamoja na Mrwanda.
Kocha wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Jules Acorse amesema atatumia mbinu zile zile zilizo wapeleka puta Morocco na Algeria na kumfanya aongoze kundi, "siijui Tanzania, lakini kama tulivyocheza dhidi ya Algeria na Morocco na hivyo hivyo tutacheza hapa, nafikiri tunaweza kufanya vizuri hapa na tivyofanya katika michezo ya awali na sasa tunaongoza kundi" alisema Acorse.

Kwa upande wa Taifa Stars, kocha Jan Poulsen amezidi kungoa safu ya ushambuliaji kwa dhumuni ya kupata magoli mengi. Poulsen amekuwa akimpatia maelekezo mara kwa mara mchezaji chipuki Mbwana Samata na huenda hapa kesho akaanza sambamba na Machupa.
Katika mchezo wa kesho mashabiki huenda waka kosa mashuti ya mbali ya Nizar Khalfan na Abdi Kasim Babi pamoja na Danny Mrwanda. Babi aliipatia goli Taifa stars katika mchezo wa kwanza dhidi ya Algeria kwa mpira wa faulo. Nizar anakumbukwa sana katika safari ya kuelekea Ghana kwa mikwaju yake ya mbali huku Mrwanda kwa goli lake maridadi pale Taifa stars walipolala na Cameroon.
Nyota hao watatu wanaokipiga nnje ya nchi watakosekana kutokana na barua za kuwaombea ruksa kushindwa kuzifikia klabu zao.
Kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Angetile Osiah, uwezekano wa wachezaji hao kuwepo katika kikosi cha Taifa Stars katika mechi ya kesho ni hafifu kufuatia taarifa za kuwaombea ruhusa walizotuma kwa klabu zao kutofika. "Tunashanga hatujui kimetokea nini kwa kina Mrwanda, Kassim na Nizar kwa sababu barua za kuwaombea ruhusa katika klabu zao hazijafika hadi sasa wakati njia iliyotumika kuwatumia tiketi ni hiyo hiyo, hivyo tunatakiwa kuwaamini wachezaji waliopo kwani huwezekano wa kuwapata tena haupo," alisema Osiah mbele ya waandishi wa habari.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.