TFF

Nyota wa Tanzania waanza kuwasili.

aamsuni
Nyota wa Tanzania wanao sakata kambumbu nje ya nchi wanatarajiwa kuwaanza kuwasili leo kwa ajili ya kuwa kabili timu ya Taifa ya jamhuri ya afrika ya kati.
Beki Idrissa Rajabu anayekipiga Sofapaka ya Kenya anayetarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo, wakati Henry Joseph anayechezea Kongsvinger Il ya Norway, Abdi Kassim na Dan Mrwanda wanaochezea DT Long An,Vietnam pamoja na Athuman Machupa anayechezea Vasalund If ya Sweden wanatarajiwa kuwasili kesho.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, kiungo Nizar Khalfan anayechezea Vancouver Whitecaps ya Canada anatarajiwa kuripoti kambini Alhamisi.
Wambura alisema wachezaji wengine wa Taifa Stars ambao walikuwa na Simba jijini Lubumbashi, walitarajiwa kujiunga na wenzao jana.

Kwa mujibu wa Wambura timu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itawasili nchini kwa mafungu kutokana na baadhi ya wachezaji kuja moja kwa moja wakitokea nchi wanazocheza soka. Alisema wachezaji hao walitarajiwa kuwasili Dar es Salaam kuanzia jana na kuwa maandalizi mengine ya mchezo huo yanaenda vizuri.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.