aamsuni
Kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars wakati anachukua timu alitoa ahadi mbili ambayo moja ameshaitimiza ambayo ni kuchukua kombe la Challenge ambalo kalichukua mwishoni mwa mwaka jana.
Ahadi nyingi aliyotoa ni kuhakikisha timu ya Taifa inafuzu kwenye kombe la mataifa Afrika, ambayo yatafanyika equatorial Guinea na Gabon hapo mwakani.
Kampini za kufuzu ziliingia dosari baada ya kufungwa goli moja na Morocco, Taifa baada ya kutoka sare na Algeria. Leo jeshi la Poulsen litakuwa na kazi ya kufufua matumaini kwa kusaka ushindi mbele ya vinara Jamhuri ya Afrika ya kati hii leo.
Jeshi hilo linalo ongozwa na nahodha Shadrack Nsajigwa 'Fuso' watakuwa kwenye uwanja wa Taifa mbele ya mashabiki wao kuwakabili timu ngumu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Timu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mechi zake mbili, haija ruhusu nyavu zake kugusa kwani walitoka sare ya bila kufungana na Morocco kisha wakailaza Algeria magoli mawili kwa bila.
Taifa stars ambayo itawakosa wachezaji wake watatu Nizar, Mrwanda, Abdi Kassim, itakuwa na kazi ya kuipenya ngome hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment