TFF

Samatta aleta mvutano

aamsuni
Uwezo wa Mbwana Samata katika kufumania nyavu umemfanya ajipatia namba ya kudumu katika kikosi cha simba sc, baada ya kupewa nafasi katika mechi zidi ya timu iliyomkuza Africa lyon.
Mbwana Samata alisajiliwa na Simba tangu mwanzoni mwa msimu huu 2010/11, ila alianza kuitumikia klabu hiyo katika mzungo wa pili, baada ya kugoma kwa madai ajatimiziwa vipengele vya mkataba.
Mchezaji huyo aliitwa katika kikosi cha Vijana stars (u23 ya Tanzania) kujiandaa na mchezo dhidi ya Cameroun, lakini mpaka sasa hajajiunga na wenzake kambini. Kutokana na hilo kocha wa timu hiyo Julio alisikika akimtaja kama mtovu wa nidhamu kwa kushindwa kuripoti kambini kwa sababu ana majukumu ya klabu.
Uwongozi wa simba, kupitia kwa afisa habari wake, alisema kuwa taratibu za kumuombea ruksa ya Mbwana Samata zimefuatwa, na kwamba Samata ajaonyesha utovu wowote wa nidhamu, alisema afisa huyo.
Mbwana Samata amekuwa mwiba kwa mabeki na makipa wa Tanzania baada ya kutikisa nyavu mara 6 katika mechi 7 za ligi kuu alizocheza.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.