TFF

Samatta, Kado, Machupa ndani

aamsuni
Jana kocha wa taifa stars Poulsen alitangaza kikosi kitakacho ivaa Africa ya kati hapo machi 26 katika dimba la Taifa. Katika kikosi hicho cha nyota 23 hawamo Kelvin Yondani 'Vidic' pamoja Salum Machaku waliokuwa nguzo muhimu katika michuane ya tusker chalenge cup hapo mwaka jana.
Katika kikosi hicho kitaendelea kukosa sura ya Jerry Tegete (yanga) na Mussa Hassan Mgosi (simba). Huku akimjumuisha mchezaji chipukizi alitemwa kwenye kikosi cha Vijana Stars Mbwana Samatta, na kipa Shabani Kado ambaye yumo kwenye kikosi cha vijana stars.
Poulsen kwa mara ya kwanza amemwita kiungo Mwinyi Kazimoto pamoja na kipa Shaban Dihile. Pia kamjumuisha mshambuliaji mkongwe anaekipiga Sweden Athuman Machupa.
Kikosi kamili kilichotangazwa jana mbele wa Wanahabari ni makipa Shaaban Kado(mtibwa), Juma Kaseja (simba) na Shaaban Dihile (Jkt ruvu) wakati mabeki ni Shadrack Nsajingwa (yanga), Aggrey Morris (Azam fc), Nadir Haroub'Canavaro' (Yanga), Stephano Mwasika (yanga), Haruna Shamte (Simba), Juma Nyoso (simba) na Idrisa Rashid (Sofapaka, kenya). Viungo ni Nurdin Bakari (Yanga), Shaaban Nditi (mtibwa), Jabir Aziz (azam fc), Henry Joseph, Abdi Kassim Babi na Mwinyi Kazimoto (Jkt ruvu) huku washambuliaji ni Dan Mrwanda, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa (azam), Mohamed Banka (simba), Athumam Machupa, John Boko (azam) na Mbwana Samata (simba).

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.