TFF

TFF Kukutana

aamsuni

Mkutano mkuu wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unatarajiwa kufunguliwa leo saa tatu asubuhi kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisama mkutano huo utafunguliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi, huku ukiwa na ajenda 16.
Mkutano huo wa Tff utamalizika kesho, huku wajumbe wote wa mkutano huo wameshawasili jijini.
Ajenda za mkutano ni Kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kusoma na kuthibitisha ajenda, kuthibitisha muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu uliopita, yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita.
Ajenda nyingine ni hotuba ya Raisi, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama, kupitisha taarifa za utekelezaji wa Kamati ya Utendaji, kupitisha taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2011, uchaguzi wa nafasi zilizo wazi, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya TFF (kujadili mikoa mipya), kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na wanachama au Kamati ya Utendaji, Mengineyo na Kufunga kikao.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.