TFF

Ballack kuikosa bafana bafana

aamsuni:

Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa stars' mwishoni mwajuma wataikaribisha timu ya taifa ya South Africa ' Bafana bafana' katika mchezo wa kirafiki utakao chezwa katika uwanja wa Taifa.
Mchezo huo utakao pigwa tarehe 14 mwezi huu, utakosa baadhi ya nyota katika timu zote mbili. Bafana bafana watakosa huduma ya Stephen Pinnar anayekipiga Tottenham nchini Uingeleza wakati Tanzania wakikosa hudumu ya viungo Nizar Khalfan na Abdi Kassim Babi 'Ballack wa Unguja' pamoja na mshambuliaji Danny Mrwanda ambao watakuwa na kibarua katika klabu zao.
Taifa stars uwenda ikawakosa pia Henry Joseph, Idrisa Rajabu pamoja na Athuman Machupa ambao wote wanacheza soka nnje ya nchi.
Wakati huo huo Bafana bafana wanatarajiwa kutua nchini kesho jioni na msafara wa watu 30, huku 10 wakiwa ni viongozi pamoja na benchi la ufundi wakati 20 wakiwa wachezaji wanaokiunda kikosi hicho.
Tiketi za pambano hilo zitaanza kuuzwa kesho tarehe 12 katika vituo vya premier betting (kariakoo- mtaa wa sukuma, Buguruni sokoni, Manzese Midizini, JM Mall na Tandale kwa Mtogole) shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa, Steers (mtaa wa Ohio na Samora), Big Bon Msimbazi (Kariakoo) na uwanja wa Uhuru.

MBWANA SAMATA AMWAGA WINO MAZEMBE.
Mbwana Samata amesaini kuitumikia klabu ya Soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Congo na anatarajiwa kupata 90mil kwa mwaka.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.