Baada ya kichapo: Simba tifuani
Baada ya kichapo cha jana kumeripotiwa kuwa ndani ya Simba hali si shwari, huku kwa wapinzani wao Yanga, wachezaji kujazwa noti.
Msemaji wa Simba akizungumza na Radio One alikanusha tukio lililotokea jana, mara baada ya mchezo kumalizika ambapo kuliripotiwa kwa Mchezaji Haruna Moshi Boban kumtwanga kichwa Mganda Emanuel Okwi.
Msemaji huyo wa Simba alisema kambi ya wachezaji ilivunja jana mara tu baada ya mchezo kumalizika ndio maana Boban alionekana akitokomea bila ya Bus la timu ambalo liliwabeba wachezaji waliokuwa wanaelekea maeneo ya Posta.
Wakati huo huo Uhuru FM iliripoti kuwa Friends Of Simba na mashabiki wa Simba walimpokea Haruna Moshi kama Shujaa baada ya kumtwanga kichwa Emanuel Okwi mbele ya Polisi ambao walishindwa kumtia nguvuni.
Uhuru FM iliripoti pia Mashabiki wa Simba wanadaiwa kumpiga Polisi, huku wakimrushia lawama Kocha wa timu hiyo kama chachu ya kupoteza mchezo huo.
Vile vile kunadaiwa kiongozi mmoja wa simba alinaswa mazungumzo yake dhidi ya wachezaji wawili wa wa yanga na kuwataka wacheze chini ya kiwango katika mchezo huo wajana na kuwa angewazawadia vigai na mabasi wachezaji hao.
Kwa upande wa yanga msemaji wa Yanga Luis Sendeu alisema uongozi wa yanga huko mbioni kuwatunuku wachezaji wao kwa kazi kubwa waliyo ifanya hapo jana kwa kuwasimamisha Simba.

0 comments:
Post a Comment