Simba Bingwa Uhai Cup
Kwa mara ya kwanza kikosi B cha Simba kimetinga fainali ya michuano ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara (Uhai Cup) na kwa mara ya kwanza wamelitwaa kombe hilo hii leo.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Karume Saa 3 asubuhi baina ya Simba na mabingwa mara mbili Azam FC ulizishuhudia timu hizo zikimaliza dakika 120 bila kufungana. Changamoto ya mikwaju ya penati ndio iliyompatia Simba ubingwa, kwa penati 5-4.
Simba wamefanikiwa kulitwaa kombe hilo linalo dhaminiwa na Kampuni inayomiliki wa Azam FC Bakhresa kupitia kinywaji cha Uhai, huku wakifanikiwa kulipa kisasa kwa Azam FC ambayo iliwavua ubingwa wa michuano ya vijana iliyoandaliwa na kituo cha Rolling Stone Mkoani Arusha.
Michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya nne kukishuhudi Simba na Ruvu Shooting wakitwa kombe hilo mara moja moja kwa kila timu huku Azam FC walioingiza wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 wakilitwaa mara mbili.
Mshambuliaji wa Azam FC, Simon Happygod Msuva ameibuka mfungaji bora na golikipa wa Azam, Aishi Mfula amekuwa golikipa bora wa mashindano. Huku Serengeti Boys ambayo inawachezaji wa 5 wakutumainiwa wa Azam Academy wakichukuwa nafasi ya 3.
1 comments:
Hongereni sana Simba kwa kuchukua Ushindi, kwani mmeonyesha ujuzi wenu na jitihada zenu zote mpaka kufikia hapo, muendelee na moyo huo huo wa ushindi.
Pia kuna link's za kitanzania mbalimbali hasa za michezo kwenye : http://www.tanzaniakwetu.com
Post a Comment