Mchangani

Mwaka wa pili wa MUM watinga fainali


Jioni ya leo katika viwanja vya Chuo Cha Kiislamu Morogoro 'MUM' kulikuwa na mtanange wa nusu fainali ya mashindano yanayoendelea hapo Chuoni, ambapo wanafunzi wanao chukua masomo ya Sayansi waliwakabili wenzao wa Mwaka wa pili wa masomo ya Sanaa.

Katika mchezo huo uliovuta hisia ya Wanachuo uliamriwa kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1 yaliyotiwa kimiani katika kipindi cha kwanza baada ya wafungaji kuwazidi ujanja mabeki watimu pinzani.

Katika kipindi Cha pili kiungo mtibuaji wa Sayansi alizawadiwa kadi nyekundu kufuatia faulo ya makusudi kwa kiungo mchezeshaji ambaye kwa mtazamo wangu ndiye mchezaji bora wa mchezo aliyefahamika kwa jina la Messi.

Katika kipindi cha kwanza wanafunzi wa mwaka wa pili walitikisa nyavu mara mbili lakini mwamuzi wa mchezo aliyakata magoli hayo na kuzua utata ambao ulizimwa kwa kumuacha mwamuzi aamue mchezo.

Kipute pute kingine kilijiri katika penati ya mwisho kwa wanafunzi wa sayansi ambayo iliwatoa nnje ya mashindano, baada ya refa kuamuru mpigaji aliyepata penati hiyo, kurudia na kukosa, na hivyo kuwapeleka mwaka wa pili fainali kwa mikwaju ya penati 5-4.

Ni kama refa angekuwa anachezesha michezo ya mitaani basi kwa uwamuzi ambao mashabiki wengi hawakuupenda, akichezea kichapo ama kutoka kiwanja kwa msaada wa polisi.

Kwa mujibu wa refa juu ya magoli aliyoyakataa ya mwaka wa pili ambao wametinga fainali, anasema goli la kwanza ambalo lilipatikana kwa mpira wa kona na kuungwa kwa ustadi kwa kichwa, mpigaji alipiga bila ridhaa yake.

Na lile la pili ambalo lilikuwa la adhabu, refa anasema ilitakiwa isipigwe moja kwa moja kama mpigaji alivyo upiga mpira na kuzama, langoni.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.