gofu

Gofu Taifa wapata viongozi wapya

MCHEZAJI Paul Matthysen amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Klabu ya TPC Moshi, Kilimanjaro jana.

Akizungumza kutoka Moshi baada ya uchaguzi huo, Ofisa Tawala wa TGU, Sophie Nyanjera alisema Matthysen amepita bila kupingwa kwa kupata kura zote 16 zilizopigwa.

Awali Matthysen alikuwa akishikilia wadhifa huo kwa muda tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Dioniz Malinzi baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) mwishoni mwa mwaka jana.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Foti Gwebe amepita katika nafasi ya makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 11 huku tano zikisema hapana. Alikuwa mgombea pekee kwenye nafasi hiyo.

Alisema katika nafasi ya Katibu, Mohamed Sadiki amepita bila kupingwa. Sadiki ambaye alikuwa kwenye uongozi uliomaliza muda wake amechukua nafasi hiyo baada ya kuombwa.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.